Na Mwandishi Wetu
Katika kutimiza majukumu yake na ahadi ya saba ya uanachama wa chama cha mapinduzi yakuwa "nitashirikiana na wenzangu wote kujenga nchi yetu" Ndugu Abrahaman Kinana katibu mkuu wa chama cha mapinduzi amekuwa mfano bora na wakuigwa na kila mwana ccm hususa vijana ambao ndiyo nguvu ya leo.
Pongezi zangu kwa Katibu mkuu taifa Ndugu Abrahaman Kinana zinaambatana na wito kwa vijana wenzangu ndani ya chama cha mapinduzi kuiona njia aliyopita na anayopita katibu mkuu huyu wa chama taifa.
Moja vijana ndani ya chama cha mapinduzi tujifunze kushiriki katika shuhuli za kijamii kwa vitendo kama afanyavyo Ndugu Kinana katika ziara zake.
Pili haina budi kwa vijana kutambua kuwa uongozi ni vitendo bila vitendo wananchi hawawezi kukupa dhamana hii ya kuwaongoza, hivyo basi vijana ndani ya chama cha mapinduzi haina budi tukawa na wingi wa vitenda zaidi ya maneno makavu.
Tatu tusiisahau asili yetu na kuibeza, Ndugu kinana ametupa mwanga katika hili, yeye japokuwa amekabidhiwa dhamana kubwa ya kuwa katibu wa chama taifa lakini bado hajadharau pale alipotokea na wala haoni haya kushiriki shuhuli za kijamii.
Kwa haya mambo muhimu matatu haina budi kwa vijana wote wa ccm na taifa hili kwa ujumla kukubali kujifunza na kuyafanyia kazi kwa vitendo ili kuuboresha ustawi wa chama chetu na taifa kwa ujumla, tukumbuke wahenga walisema maneno makavu hayavunji mfupa.




0 comments:
Post a Comment