Tuesday, August 9, 2016

>>> >>>

HOJA YA TUNDU LISU 'DIKTETA UCHWARA' NI KUTETEA WAHUJUMU UCHUMI

Imechapwa na: UV MAPINDUZI - 6:19 PM
Na Comrad Bambino
Nimejiuliza kwa muda mrefu hoja ya raisi kuwa DIKTETA tena ikiongezewa neno UCHWARA ni hoja yenye lengo gani kwa taifa? Labda tuijadili.
Kwanza tupate tofauti na hasa vyanzo vya mtu kuwa dikteta kama kiongozi wa nchi. Kiongozi anaweza kuwa dikteta kwa kuipindua serikali iliyopo madarakani, kung'ang'ania madaraka muda mrefu na kwa kuto kuitisha uchaguzi mkuu kwa nia ya kubaki madarakani. Duniani hakuna kiongozi anayetuhumiwa dikteta kwa kuisimamia misingi halali(sheria) bila kuhusisha sababu tajwa juu, isipokuwa Tanzania pekee. Pengine mtu akatahamaki na kusema anakandamiza demokrasia kama anavyosema na kujitetea Lisu lakini swali la msingi ni kwa namna gani raisi JPM anakandamiza demokrasia, je raisi JPM ameshafikisha muda wake kikatiba wa kumaliza uongozi akang'ang'ania kubaki madarakani?, au ni kwa kuwaambia watanzania kuwa muda wa siasa (kampeni) umekwisha sasa ni kufanya kazi ndio inahalalisha kuwa ni dikteta?. Lakini embu tulitafakari neno hili dikteta uchwara kwa kina ili kupata mwanga wa nini kilimsukuma Lisu kusema kauli hiyo. Neno uchwara kwa mimi nijuavyo linamaanisha mkosi, nuksi au balaa. Ninapolichukua neno dikteta napata maana ya matumizi ya nguvu au mabavu. Lakini kila nikiyaunganisha maneno haya kuipata mantiki ya hoja hii yenye kuendana na hali ya kimazingira kwa sasa nchini napata maana " utumiaji nguvu ulioleta balaa!" hapa ndipo napata swali kwanini baadhi ya watu wanatumia neno hilo kumdhihaki kiongozi wa taifa.
Raisi JPM alipokuwa akiwania uraisi alionesha wazi hari ya kushuhulikia uhujumu uchumi nchini kazi aliyoianza na kuendelea nayo ambayo kwa baadhi ya watu imegeuka kuwa balaa na nuksi kubwa hata kufikia hatua kumfananisha na mtu aliyetumia nguvu (sheria) kuwaletea balaa hilo.
Ni kutokana na mantiki ya neno hilo kimazingira na diriki kusema Lisu kumuita raisi dikteta uchwara anatetea kama si kutumika na wahujumu waliopata balaa hilo la matumizi ya sheria za nchi. 
Pale mtu anapo ongelea raisi wa taifa kama dikteta yampasa kuwa na vielelezo vinavyotambulika kimataifa ikikumbukwa kuwa Tanzania haipo pekeyake duniani kuna mataifa na mashirika ulimwenguni yenye maadhimio na mikataba inayopinga udikteta. Lisu kama msomi wa sheria ni wazi kuwa anajua dhahiri udikteta uchwara anaoutuhumu haupo hata kwenye orodha na vigezo vya raisi kuwa dikteta kimataifa, Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa. 
Hivyo ni wazi mwanasiasa huyu anachochea chuki, na hofu kwa watanzania juu ya raisi wao. 
** Kuchochea, kuunga mkono na kushiriki ghasia na vurugu za aina yoyote kwenye taifa lolote ni kuhalalisha ubakwaji na ukatili kwa mama, dada na watoto wetu wa kike, amka mtanzania tambua nafasi yako kulijenga taifa na kudumisha amani**
______________________
MakalaZaNyumbani

Shirikisha

& Hoji

0 comments:

Post a Comment

Download It from Here

MonotataPx I Mbinotrix I MonotataPx I Mbinotrix