Tuesday, August 9, 2016

>>> >>> >>>

SERIKALI KUHAMIA DODOMA NA HOJA BUTU ZA UPINZANI.

Imechapwa na: UV MAPINDUZI - 6:32 PM
Na Comrad Bambino 
Nianze kwa kusema Mwenyezi Mungu ampe pumziko la amani Mwl. J. K. Nyerere. Kwanini basi nimeanza na kauli hiyo kabla ya salamu? ni kwasababu ya umuhimu wa kiongozi huyu na mchango wake kwa yale watanzania waliyoyaitaji na wanayozidi kwa kasi kuyahitaji na kuyatafuta. Ndugu yangu habari za wakati huu?, leo nimekusanya akili zangu ili niweze kushiriki jambo na wewe mtanzania mwenzangu kuhusi hili swala haswa la serikali kuhamia mjini Dodoma mapema kabla ya 2020 ikiwa ni kutekeleza tamko/agizo la raisi wa jamhuri Ndg. J. P. Magufuli.
Binafsi naunga mkono nia njema ya serikali ya awamu ya 5 ya kutaka na kuendelea kutimiza azima ya mwasisi wa taifa letu Mwl. Nyerere ya serikali kuwepo mjini Dodoma.
Japo zimetolewa hoja nyingi zenye kupinga swala hili nyingine zikitolewa kwa nia na dhati ya mioyo huku nyingine zikitolewa kwa matakwa ya kisiasa huku nyingine zikitolewa ama ikiwa ni hulka ya baadhi ya watu au mtu mmoja mmoja, zote hizo tunaziita hoja ambazo pia ni hoja za watanzania wenye haki hiyo kikatiba. Lakini embu basi tuzipime na kuzichambua hoja hizo je, zina mashiko au ndio kwa vile tuna uhuru wa maoni na demokrasia hiyo hoja zinaweza tolewa.
1. Serikali imekurupuka!, hoja hii ni hoja yakushangaza, kwanini ni hoja ya kushangaza? Wengi wa wanaotoa hoja hii wanashindwa kukumbuka kuwa lengo la serikali kuwa Dodoma halijaanza 2016 na Dk. Magufuli bali lengo hili lilianza na Mwl. Nyerere miaka ya 1970. Hivyo mtu kusema serikali imekurupuka ni dalili za ama mhusika ndiye kakurupuka kutoa hoja hiyo au la hajui alisemalo au kaamua tu kusema akidhani ndivyo yampasa kusema hasa kisiasa. 
2. Hoja ya Dodoma kuwa na zuio la kujenga majengo marefu (magorofa), pia hoja hii endapo itachukuliwa haraka haraka yaweza onekana yenye mashiko lakini La! Hoja hii kama ya awalu nayo inakosa nguvu hasa pale linapokuja swali la kwanini eneo fulani huwa na magorofa? Kazi yake ni nini?, je mji ili uwe mji lazima uwe na magorofa?, kwa ufupi tu, majengo hayo hujengwa pale panapokuwa na watu wengi kuzidi uwezo wa eneo hususa makazi ya watu, leo hii watumishi na ofisi za serikali watakao kwenda Dodoma je, watakuwa wengi kiasi cha kuzidi wanafunzi wa chuo kikubwa kama UDIM? Kama jibu ni hapana, je wanafunzi hao wa UDOM wamechukua eneo kiasi gani cha Dodoma?. Kwa maswali hayo hoja hii tena iliyotolewa na mbunge(jina nahifadhi) haina mashiko bila shaka hakutafakari alichosema.
3. Lengo la kuhamia Dodoma haikuwa kwenye ilani ya CCM 2015/20. Jamani hadi hili? sasa kila swala liwe kwenye ilani hata yale yaliyokuwepo tangu kale.
4. Ramani ya Dodoma haikidhi mahitaji ya sasa (ramani ni ya zamani), hahah!! Kila nikisikia hoja hii huwa ninacheka, kwanini basi? Kwasababu kwanza hoja hii haiendani na ukweli kivipi basi wapo watakaosema hoja hii ni kweli ramani ya tangu Mwalimu, sawa lakini kwanini nimesema haiendani na uhalisia, ni kwasababu ramani ya Dodoma si ramani ya nyumba moja, ni ramani ya mji, pili lengo la ramani ya Dodoma bado ni lile lile kuwa mji mkuu, tatu ramani ya Dodoma ni ramani ya mji ambayo hata haijafikisha miaka 50, ki vipi basi, kuna miji mikongwe duniani na bado ina gadhi kubwa kidiplomasia na kadhalika mfano miji kama Viena, Paris, Washington,Moscow, London n.k hoja ya uzee au ukongwe wa ramani ya Dodoma kutokidhi hali ya sasa inakosa mashiko pia.
Hivyo nini kifanyike basi, binafsi nazidi kuipongeza serikali ya Dk. Magufuli kwa azma yake, pia nazidi kuwasisitizia ndugu zangu hususa wanasiasa upinzani kuwa si kila jambo lakupinga mengine ni yakushirikiana kwani Tanzania si ya CCM wala UKAWA au chama kingine chochote bali Tanzania ni ya watanzania mimi na wewe ambao jukumu letu ni kuiendeleza kwa kukuza uchumi wake.
_______________________
‪#‎MakalaZaNyumbani‬

Shirikisha

& Hoji

0 comments:

Post a Comment

Download It from Here

MonotataPx I Mbinotrix I MonotataPx I Mbinotrix