Na
Comrad Bambino .
Kila
ifikapo mwezi wa nne taifa huzizima kwa masikitiko na majonzi likiwakumbuka
mashujaa wake wawili Ndugu Abeid Karume mwasisi mpambanaji na kiongozi wa
mapinduzi ya wengi visiwani Zanzibar ambayo ndiyo yalileta uhuru wa kweli kwa
waafrika wazanzabari na Ndugu Edward Sokoine aliyekuwa waziri mkuu wa Jamhuri
ya muungano Tanzania mwaka 1977 hadi 1980 kishakurudi tena ofisini mwaka 1983
hadi mwaka 1984.
Hawa
walikuwa viongozi mashujaa kabisa katika historia ya kuleta maendeleo katika
nchi yetu. Tukianza na Ndugu Abeid Karume aliyekuwa raisi wa kwanza wa Zanzibar
kiongozi wa mapinduzi yaliyoleta ukombozi wa wengi visiwani Zanzibar. Abeid
Karume atakumbukwa kwa mengi visiwani Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.
Hayati
Edward Sokoine naye atakumbukwa kwa mengi kama mzalendo mpigania maendeleo
Tanzania, ni kweli isiyofichika kuwa hayati Sokoine alikuwa waziri mkuu wa
Tanzania aliyekuwa na ndoto kubwa ya maendeleo ya taifa letu. Akiwa mzalendo
aliye bobea katika siasa za usawa wa kibinadamu na ujamaa hayati Sokoine
alionekana kama nuru ya maendeleo ya taifa letu.
Kwenye picha ya kulia ni baba wa taifa Mwl. Julius K. Nyerere akimsikiliza kwa umakini hayati Edward M. Sokoine katika moja ya majukumu ya kimaendeleo aliyokuwa akiyasimamia, Chini kushoto ni waasisi wa taifa letu hayati baba wa taifa Mwl. Julius K Nyerere na hayati kiongozi wa mapinduzi Zanzibar Abeid Karume katika moja ya majukumu muhimu ya taifa letu.
Kweli Chema hakidumu! Leo hatupo nao tena wazalendo waleta maendeleo ya taifa letu wametutoka wapambanaji hawa waliokuwa nuru ya maendeleo ya taifa letu. Tuzidi kuwaombea wazalendo hawa na wazalendo wengine wote wa taifa letu wapumzike mahala pema peponi Ameni!.
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)

0 comments:
Post a Comment