Sunday, April 19, 2015

>>> >>> >>> >>>

MAADHIMISHO MIAKA 60 YA JUMUIYA YA WAZAZI CCM, BULEMBO AWATAHADHARISHA MBIO ZA URAISI OCTOBA

Imechapwa na: UV MAPINDUZI - 4:53 AM
Na Mwandishi Wetu

Jumuiya ya wazazi chama cha mapinduzi una adhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwake, wiki ya wazazi CCM ime adhimishwa rasmi mkoani Mbeya kitaifa. Akipokea taarifa ya Mkoa Mbeya mara baada ya kuwasili mkoani hapo Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi taifa Ndugu Alhaj Abdallah Bulembo alizungumzia suala la mbio za kuwania nafasi ya kugombea uraisi ndani ya chama na kutoa msimamo wa jumuiya ya wazazi.

Alisema kuwa wapo baadhi ya wawania nafasi hiyo ya kupeperusha bendera ya chama Oktoba walioanza kueneza uvumi kuwa jumuiya hiyo inawaunga mkono katika harakati zao za kutafuta uungwaji mkono, jambo ambalo si la kweli.

“Jumuiya ya wazazi itamuunga mkono mgombea wa CCM aliyepitishwa na chama kupitia vikao halali, wale wanaodhani kuwa wanaweza kuitumia jumuiya hii kama ngazi ya kufanikisha malengo yao watambue kuwa hilo haliwezekani” alisisitiza Ndugu Bulembo

Pia Ndugu Bulembo  alizidi kusisitiza kuwa jumuiya ya wazazi inakutana mjini mbeya ili kuadhimisha wiki ya jumuiya hiyo, kutafakari sera ya maadili na wala si kwenda kumpigia debe mtu yeyote ndani au nje ya chama. Hata hivyo hakukataza wanachama wa jumuiya hiyo kumuunga mkono mtu  yeyote ndani ya chama kwani hilo litakuwa ni swala la  mtu binafsi wala siyo jumuiya.


Awali akisoma taarifa ya chama mkoa wa mbeya katibu wa chama mkoa alisema kuwa kitendo cha jumuiya hiyo kufanya maadhimisho hayo mkoani Mbeya ni sawa na kuandika historia kwa mkoa huo kwani  taifa linataraji kukutana na matukio mawili makubwa ambayo ni kupatikana kwa katiba mpya pamoja na uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge na raisi.

Shirikisha

& Hoji

0 comments:

Post a Comment

Download It from Here

MonotataPx I Mbinotrix I MonotataPx I Mbinotrix