Monday, January 16, 2017

>>>

HII NDIO LUGHA RAHISI - TUWAPUUZE WANASIASA KAMA LOWASSA.

Imechapwa na: UV MAPINDUZI - 10:57 AM

✍Na Menuka Jr.
Imeandikwa, "Hakuna mwanzo haramu wenye Mwisho harali" Hakuna, ukianza hovyo utamaliza hivyohivyo, huo ndio utaratibu!

Unaweza kuzungumza ukiwa Kanisani ktk Mimbari, ukiwa Bukoba Mjini au kokote utakapo lkn kama maneno yako yameharibiwa na tamaa za mwili na Dunia, hakuna lolote, umeliwa tu!

Tarehe 15 January 2016 (jana), Edward Lowassa  akiwa Bukoba Mjini, kwa sauti yake ya kunong'ona amesikika akisema kuwa atawaletea Wananchi wa Bukoba Chakula,kwamba ataomba kwa marafiki zake nje ya Nchi na watamuelewa!
Lowassa na wenzake hapa hesabu umewashinda, wameliwa!

Kuna Watu wanaweza kumuelewa Lowassa kuwa amekusudia kuwasaidia Wananchi wa Bukoba. Kwamba, anaguswa na matatazo yao hivyo anaungana nao. Wenye kuamini hili waanze kufanya kazi kwa sababu watachelewa tu,hakuna Chakula cha Lowassa.
Kama wewe ni kati ya Watu wa namna hii, wanaomuamini Lowassa, basi, umeliwa! 
Labda sio Lowassa yule wa Richmond na Uanglikanism.
Wananchi wa Kagera wanatakiwa kujua kuwa Lowassa hakuwahi kuwa na huruma na Wanyonge wa Nchi hii tangu amezaliwa. Lowassa hakuwahi kushirikiana na Maskini wa Tanzania kwa sababu hakuna urafiki kati ya Tajiri na Maskini. Lowassa tangu kuzaliwa kwake amekuwa akiwaza faida tu,Lowassa ni Mtu wa dili, full stop!

Hatuhitaji tarakimu kuthibitisha hili. Ktk historia ya Nchi hii hakuna mahala kokote ambako Lowassa amewasaidia Wanyonge zaidi ya kuwaibia na kuwadhurumu Rasilimali zao kwa ujanjaujanja.

Kuna Watu kwa kutokumjua Lowassa vizuri wanaweza kujidanganya kuwa alipokuwa Waziri Mkuu, Lowassa alisimamia ugawaji wa Chakula Nchini. Kama ni mmoja wao umeliwa! Humjui Lowassa vizuri.
Mbwembwe zote zile kule Shinyanga na Cheni shingoni, Arusha na kwingineko alikofika kusema Chakula, Lowassa alikua akiratibu harakati zake za Urais wa 2010. Lowassa hakufanya yote yale kwa utashi wake na Uchungu kwa Wananchi isipokuwa Urais wa JMT. Kwa Lowasa Urais ni muhimu kuliko jambo lolote! Kwake ile ilikuwa mbinu ya kumuweka karibu na Wananchi Wanyonge, aonekane mwenye huruma ili wakati utapofika atimize haja yake. 

Kwa bahati mbaya sana, Lowassa amekuwa akirudia mbinu zilezile na Watu walewale. Kama kuna watu Kagera wanadhani kuwa Lowassa anaguswa na janga la Kagera, basi Mtu huyo anajidanganya kabisa!
Hilo la Chakula Kagera kwa Lowassa halipo na haliwezekani, kwa sababu Lowassa hiyo mamlaka hana! Anajua wazi kuwa hawezi kuingiza Chakula Nchini kwa kisingizio cha Njaa ya Bukoba! Njaa ktk Nchi ni baa(Janga). Uko utaratibu wa Serikali wa kushughulika na Majanga yanapolikumba Taifa sio kwa porojoporojo kama za Lowassa.

Kilichofanyika Kagera ni kuwahadaa Wananchi wa Kagera ili wasifanye kazi zao wategemee msaada ambao kimsingi haupo! Lowassa bado anazo ndoto za kuwa Rais wa Nchi hii ifikapo 2020, kwa hiyo anatumia nafasi hii ya matatizo yetu kujiandaa na Urais wake.

Watu wa Kagera tumpuuze Lowasa tufanye Kazi kwa Maendeleo yetu. Tusikubali kubabaishwa na Wanasiasa wenye nia ovu ktk Nchi yetu!
Tunaweza kuandika insha ndefu, maneno mengi na mengi lkn lugha rahisi kabisa kwa Maendeleo yetu ni kufanya Kazi na  kuwapuuza Wanasiasa kama Edward Ngoyai Lowassa.
#NinamuungaMkonoRaisWangu
#NinafanyaKaziKwaMaendeleoYaNchiYangu.

Shirikisha

& Hoji

0 comments:

Post a Comment

Download It from Here

MonotataPx I Mbinotrix I MonotataPx I Mbinotrix