Na Menuka Jr.
Mambo yanayoendelea katika Nchi hii
yanaweza kukusukuma kucheka hata pale isipohitajika๐๐๐๐๐
Hivi utajiskiaje kusikia kuwa katika Nchi moja yenye Ukame Bangi zinazooteshwa na Wapinzani zinastawi wakati huohuo
Chakula kinachooyeshwa na Wananchi kinakauka?
Ni Wiki mbili sasa Wanasiasa wa
Nchi yetu hasa Wapinzani (ACT-Wazalendo, CHADEMA), wameamua kujitoa fahamu
kabisa ilimradi tu watimize matakwa yao kisiasa.Ni bahati mbaya sana kuwa
Wanasiasa wetu ni wasahaulifu mno! Wastani wao wa kusahau ni kilomita tatu kwa
saa yaani 3km/hr. Na kadiri muda unavyokwenda ndivyo hali inakua mbaya zaidi.
Kwa usahaulifu wao wanadhani
Watanzania wote ni mifano yao, kwamba hatuna kumbukumbu kwa matendo na taarifa
za Nchi yetu. Wameliwa! Kama unataka kunielewa vizuri kabisa, usipate taabu,
tufuatane katika tafakari hii.
Mwishoni mwa Mwaka jana huko
Arusha alikamatwa Diwani wa Kata ya Lemanyata Losyeku Kilusu
(CHADEMA),Wenyeviti Saba wa Vitongoji (CHADEMA) na Wenyeviti Watatu wa Vijiji
(CHADEMA). Viongozi wote hawa wanaotokana na
Chama cha Demokrasia na Maendeleo ya Njaa na Ukame Bandia walikamatwa
baada ya kubainika kuwa wanamiliki na kuendesha kilimo cha Bangi kwa Shamba
lenye ukubwa zaidi ya Hekali Nane. Ikumbukwe
kuwa Kilimo cha Bangi ni haramu kwa Sheria za Nchi yetu.
Ukiitazama vizuri picha ya Shamba
hilo la Bangi lilivyonawili na kustawi kwa rangi ya kijani kibichi huwezi
kukwepa kuhitimisha kuwa Ardhi ya Tanzania ni kiboko, ina rutuba ya kutosha na
maji ya kustawisha Mimea na Mazao.
Baada ya muda mfupi kupita,
Viongozi hao walima Bangi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ya Njaa na Ukame
Bandia, wameibuka na taarifa ya Njaa Nchini na Ukame wa hali ya juu. Wanasema
kuwa, hali ya Chakula Nchini ni mbaya mno kwa sababu hakuna Mvua na Mifugo
inakufa kwa kukosa Nyasi na Maji. Watu hawa kwa nia ovu kabisa, wamediriki
kutumia picha za Nchi kama Sudani na Afrika Kusini kutaka kuwaaminisha Watu wa
Nchi hii kuwa kuna ukame. Haya ni mambo makubwa mno katika Nchi.
Baada ya mambo haya pamoja na
juhudi kubwa za kulifarakanisha Taifa hili kwa kisingizio cha njaa, mimi
nimejifunza mambo kadhaa kama ifuatavyo;
Mosi, Ni Tanzania pekee ambapo
Ukame unaotesha zaidi Bangi kuliko Mazao ya Chakula ndio maana Bangi Hekali mbili zinaweza kunawili na
kustawi, lkn Mahindi na Mtama vikakauka kau.
Pili, Viongozi wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo ya Njaa na Ukame wanaweza kulima kwa ustadi Bangi
haramu lkn hawawezi kabisa kulima ama kuwashauli na kuwaongoza Watanzania ktk
kulima mazao ya Chakula.
Tatu, Ni Tanzania pekee ambapo
Ukame hutokea kama shoti ya Umeme bila ishara na ghafra mifugo mamia kwa mamia
kufariki na Mahindi kukauka huku picha zinazotumiwa zikiazimwa kutoka South
Sudan na South Afrika. Tunahitaji Maombo maalum kwa Wapinzani wa Nchi hii.
Nne, Ni Tanzania pekee ambapo
taarifa za Baa(Janga) la Njaa hazitokani na utafiti wala takwimu isipokuwa
Chaguzi ndogo za Madiwani kama Kijichi, Geita na huko Arusha kwa ajili ya
maslahi ya Kisiasa.
Tano, Ni Tanzania pekee ambapo
Janga kubwa kama linahubiriwa kisiasa kwa kuwashawishi Wananchi wasifanye kazi
kwa ajili ya Uzalishaji mali bali walalame kwa Rais na kuingoja Serikali
kutatua matatizo yao.
Kwakweli tunahitaji akili kubwa
mno kuishi na Watu wa namna hii. Wanasiasa Wachonganishi kama Zitto Kabwe na
Lowassa ni hatari mno kwa Ustawi wa Taifa letu. Hakuna Nchi ambayo imewahi
kuendelea ama kutatua Matatizo yanayowakabili kwa kuendekeza maneno bila
kufanya kazi. Ni lazima tufanye kazi kwa Maendeleo ya Nchi yetu.
#NamuungaMkonoRaisWangu
#NafanyaKaziKwaMaendeleoYaNchiYangu.


0 comments:
Post a Comment